Familia ya soka dunia nzima imeingia katika simanzi baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Senegal Bruno Metsu kufariki dunia.
Kocha huyo raia wa Ufaransa amefariki dunia kutokana na kuugua ugonjwa wa kansa ambayo ilikuwa ikimsumbua kwa muda mrefu akiwa na miaka 59.
Kocha huyo aliyepata mafanikio na timu ya taifa ya senegal katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2002 yaliyofanyika korea kusini na Japan.
Kocha huyo aliifikisha timu hiyo hadi hatua ya robo fainali na kutolewa na Uturuki kwa mfumo wa goli la dhahabu lililofungwa na Hassan Sas.
Metsu aliyewahi kuzichezea timu za Lille na Anderlecht na baadaye kuanza ukocha katika maeneo ya Asia ya kati na kuchukua kombe la mbingwa Asia na timu ya Al-Ain mwaka 2003 na Gulf cup UAE mwaka 2007 hayo mafanikio yote baada ya kuachana na timu ya taifa ya Senegal.
Hakika taifa la senegal halitasahau mafanikio waliyoyapata kupitia kocha huyo.
Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi amin.

No comments:
Post a Comment