Monday, October 14, 2013

SIR ALEX FERGUSON AIONGELEA MANCHESTER UNITED NA KUSEMA HAYA.........

Kocha wa zamani wa man united raia wa Scotland Sir Alex Ferguson ameiongelea timu yake ya zamani na kusema kwamba united itabaki kuwa timu bora katika ramani ya soka barani ulaya.

Hayo aliyasema leo  na kusema kwamba man united ni timu bora na ni kubwa na punde itarudi katika hali yake ya kawaida katika ligi kuu ya uingereza.

United hadi sasa wameshacheza mechi 8 na kufikisha point 10 na kushika nafasi ya 9 katika msimao wa ligi na huku ikijikusanyia poimt 4 katika mechi 2 za ligi ya mabingwa ulaya.

Sir Alex alisema kwamba licha ya timu hiyo kuanza kwa kusuasua katika ligi kuu  nchini humo chini ya kocha mpaya aliyetokea Everton na kuachiwa mikoba na Ferguson, David Moyes lakini anatumaini na kusisitiza kwamba mashabiki wa timu hiyo duniani kote  wanatakiwa kuwa watulivu kwani timu yao itarudi katika hali nzuri ukizingatia ya kamba wana wachezaji wazuri na wenye uzoefu katika ligi mbalimbali.

Kocha huyo wazani alimwachia Moyes mikoba yake mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kunyakuwa ubingwa wa ligi kuu ya uingereza mara 20 ambapo tayari alishafikisha miaka 71 na kuhitaji kupumzika na presha za soka na mwenyewe kumpendekeza Moyes kurithi mikoba hiyo punde baada ya kutangaza kujiuzuru ukocha.

Vilevile Sir Alex alifanikiwa kuipa mataji tofauti man united yapatayo 38 katika kipindi chote cha ukocha ndani ya timu hiyo yakiwemo makombe mawili ya ligi ya mabingwa ulaya mwaka 1999 dhidi ya beryan munich na maka 2009 dhidi ya chelsea.

No comments:

Post a Comment