Monday, October 14, 2013

XAVI AMTETEA NEYMAR NA KUSEMA HAYA....

Kiungo bora wa kati ndani ya miaka 6 sasa mwenye historia nzuri na timu ya taifa ya hispania na timu ya soka ya Barcelona Xavi Hernandez amemtetea mchezaji mwezake katika timu ya barcelona anayetokea Brazil Neymar Junior na kusema kwamba yeye si mrukaji maana ya kwamba hajidondoshi.

Hayo aliyasema baada ya vyombo vingi vya habari nchini humo vikimwandama nyota huyo kwamba anajidondosha pindi akiguswa kidogo tu na kusababisha madhara kwa wengine..

Aliongeza kwa kusema kwamba hastahili kutupiwa lawama anazopata hivi sasa kwani yeye anajilinda kutokana na majeraha aliyo yapata hivi karibuni na kupona punde tu.

"Ki uhalisia Neymar ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji kwa kweli tunajivunia kwa hilo kwa kila mwana familia ya barcelona dunia nzima na vilevile ni star kwani kila mtu humuangalia pindi awapo uwanjani" alisema Xavi.

Kiungo huyo mwenye miaka 33 alisema kwamba Barcelona wasipate presha ya kutafuta mtu ambaye atakuja kuziba pengo lake kwani anaamini huyo mtu yupo na atatokea tu pindi muda utakapowadia.

Vilevile Xavi anamakataba na timu yake hiyo yenye maskani mwake mtaa wa catalunya jijini barcelona hadi msimu wa ligi mwaka 20115-2016.

No comments:

Post a Comment