Friday, October 25, 2013

VAN PERSIEA DIMBANI KESHO NI BAADA YA KUIKOSA MECHI YA JUMATANO DHIDI YA SOCIEDAD

Kocha wa Manchester United David Moyes amebainisha kwamba mshambuliji wake tegemezi Robin Van Persie huenda akaanza katika kikosi cha kwanza kesho katika mchezo wa ligi kuu ya England dhidi ya Stoke City.

Hayo ameyasema leo baada ya mazoezi na kutegemea kwamba mshambuliaji huyo hatari kutoka Uholanzi huenda akaanza katika mchezo wa kesho baada ya kukosekana katika mchezo uliopita wa micuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Real Sociedad ambapo United ilipata ushindi wa bao 1-0 na kuongoza kundi lao kwa jumla ya pointi 7.

Nyota huyo mwenye miaka 30 aliukosa mchezo huo baada ya kuwa majeruhi na kwa sasa yuko tayari kuikabili wapinzani wao kesho katika majira ya saa 11:00 kwa masaa ya Afrika mashariki.

No comments:

Post a Comment