Friday, October 25, 2013

ROBINHO AMLILIA IBRAHIMOVIC MILAN

Nyota wa kibrazil na timu  ya Ac Milan Robinho amedai kwamba kukosekana kwa mshambuliaji mwezake wa zamani wa timu hiyo Zlatan Ibrahimovic kunaikosesha mambo mengi kwa sasa hasa baada ya kuwasili kwa Balotelli na Kaka ndani ya timu hiyo.

Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid amesema kwamba uwepo wa  nyota huyo raia wa sweeden kungeinufaisha sana timu hiyo kwa kuwa kunawachezaji wengi ambao wangeshirikiana pamoja na kufanya timu hiyo ifanye vizuri katika michuano mbalimbali.

Pia nyota huyo aliyewahi kuichezea timu ya man city ya nchini uingereza ameongeza kwamba ushirikiano wake na Balotelli ungeleta tija kubwa kwa kuwa wote wana uwezo wa hali ya juu na nyuma yao angelicheza Kaka.

Robinho mwisho wa msimu uliopita alikaririwa kwamba angeliondoka clabuni hapo na kurejea nyumbani kwao katika timu ya Santos lakini bado yuko na timu hiyo na mkataba wake wa sasa unaisha mwaka 2016.

No comments:

Post a Comment