Sunday, November 3, 2013

ARSENAL MWENDO MDUNDO, YAINYUKA LIVERPOOL 2-0 NA KUENDELEA KUKAA KILELENI

Washika bunduki wa London Arsena jana iliifanyia kitu mbaya timu ya Liverpool  kwa kuwachapa mabao 2-0 na kuendelea kukaa kileleni.


Dakika ya 19 baada ya mchezo kuanza alikuwa kiungo machachari kutoka Hispania Saintiago Carzola alifanikiwa kuiandikia timu yake bao la kwanza baada ya kupiga shuti kati kali lililomshinda kipi wa liverpool..

Baadaye kipindi cha pili kiungo aliyerudi na kasi  ya aina yake Aaron Ramsey alipofanikiwa kuitandika bai la pili kwa shuti kali la mita 25 na kumuacha kipa wa liverpool akiruka bila mafanikio.


Katika mchezo huo ambao kocha wa Liverpool aliamua kumuanzisha kinda John Flanadgan katika upande wa kulia kama beki na ndipo upande huo akina Rosisky na wezake walipokuwa wanapitia na kuonekana kupwaya.


Hata hivyo washambuliaji wa liverpool Sturridge na Suarez walijaribu kuisumbua ngome ya Arsenal lakini beki ya Arsenal ikiongozwa na Mertersacher ilifanikiwa kuwadhibiti.

No comments:

Post a Comment