Mshambuliaji kutoka Hispania Jose Callejon jana aliipa ushindi timu yake baada ya kupachika bao la pili dhidi ya Catania katika mchezo wa ligi kuu ya Italia maarufu kama serie A.
Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid alifanikiwa kufunga bao safi na la pili ikiwa kabla Merek Hamsik aliifungia bao la kwnza timu hiyo.
Kocha wa timu hiyo Rafa Benitez alizungumzia mchezo huwo na kusema kwamba ulikuwa ni mchezo mgumu kwao hasa kabla ya dakika 30 za kwanza lakini kila muda ulivyokwenda timu ikaanza kuimarika kimchezo na kuanza kumiliki na hatimaye timu ikaanza kupata matokeo.
Aliongeza kwa kusema kwamba anashukuru kwa kuwa timu yake inaanza kuimarika katika michezo mbalimbali hasa baada ya kurudi baadhi ya wachezaji ambao walikuwa majeruhi na wapo tayari kwa michuano yeyote sasa.
Akimzungumzia Callejon alisema kwamba ni mchezaji mwenye kipaji na hutaka kujifunza kila wakati na anajitahidi sana na ndio maana amefanya tulichokipata.
No comments:
Post a Comment