REAL
Madrid imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 usiku huu dhidi ya Almeria
katika Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga kwenye Uwanja wa
Estadio de los Juegos, MediterrĂ¡neos.
Cristiano
Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya tatu kwa Real Madrid pasi ya
Isco kabla ya kutolewa nje kwa maumivu ya nyama, ambayo kwa sasa
yanamuweka nje mpinzani wake mkuu katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa
Dunia, Lionel Messi wa Barcelona pia ya Hispania.
Sasa
Mreno huyo yuko shakani kuichezea Real katika mechi ya Ligi ya Mabingwa
dhidi ya Galatasaray Jumatano, ingawa baada ya mechi kocha wa Madrid ,
Carlo Ancelotti alisema: "Cristiano ana matatizo ya nyama, lakini ni
mshituko tu, hakuna maumivu makubwa,".
Karim
Benzema aliifungia Real bao la pili dakika ya 61 pasi ya Jese Rodriguez
kabla ya Gareth Bale kufunga la tatu dakika ya 71, , Isco la nne dakika
ya 75 pasi ya Jese Rodriguez na Alvaro Morata kuhitimisha karamu hiyo
ya mabao dakika ya 81, pasi ya Casemiro.
No comments:
Post a Comment