TIMU
ya soka ya CS Sfaxien ya Tunisia, Jana imeutumia vyema Uwanja wa
nyumbani, Stade Olympique de Rades baada ya kuilaza mabao 2-0 Tout
Puissant Mazembe ya DRC katika Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho
Afrika mjini Tunis.
Shukrani kwao, washambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Ibrahim Didier Ndong aliyefunga bao la kwanza dakika ya 16 na mshambuliaji wa Taha Yassine Khenissi aliyefunga la pili dakika ya 90 na ushei wakimtungua kipa mahiri, Robert Muteba Kidiaba.
Washambuliaji
wote wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu
walianza katika kikosi cha Mazembe pamoja na Tressor Mputu Mabi, lakini
hawakuweza kuwanusuru mabingwa mara nne Afrika na kipigo hicho.Sfaxien,
timu pekee iliyoshinda Kombe la Shirikisho mara mbili tangu
kutambulishwa kwa mfumo mpya mwaka 2004, yenye maskani yake katika mji
uliozungukwa na bahari ya Mediterranean, Sfax sasa itahitaji sare katika
mchezo wa marudiano Novemba 30 au kufungwa kwa tofauti isiyozidi bao
1-0, mjini Lubumbashi ili kujinyakulia taji na kitita cha dola za
Kimarekani, 625 000. Mshindi wa pili atapata dola 432 000.
Mshindi pia atamenyana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly ya Misri kuwania taji la Super Cup mechi itakayopigwa nchini Misri Februari 2014.
No comments:
Post a Comment