Kocha wa manchester united David Moyes amebainisha kwamba kesho atawakosa wachezaji wake mahiri katika safu ya ulinzi Jonny Evans na Rafael Da Silva baada ya kuumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fulham jumamosi iliyopita.
Kocha huyo amebainisha hayo baada ya washabiki wa timu kutaka hali ya nyota hao ilihali wanakabiliwa na mechi kubwa dhidi ya Arsenal mwisho wa wiki hii na kusema kwamba wataukosa mchezo huo wa jumanne yaani kesho kutokana na kuumia enka na bado haja bainisha kuhusiana na hali ya kiungo Tom Cleverly kwani na yeye alipata majeruhi katika mchezi huo ambao united ilishinda mabao 3-1na kutozungumzia kabisa hali ya wachezaji hao katika mchezo dhidi ya Arsenal.
No comments:
Post a Comment