WINGA
Gareth Bale amewathibitishia mashaiki wa Real Madrid kwamba yeye ni
mkali na guu la kushoto, baada ya jana kutoa pasi za mabao mawili katika
ushindi wa 3-2 wa timu hiyo dhidi ya Rayo Vallecano.
Wakiwa
wanaitwa Mabao ya Euro Milioni 194 mjini Madrid – Ronaldo alimalizia
pasi ya Bale na kama ilivyokuwa katika ushindi wa 7-3 dhidi ya Sevilla
kawikati ya wiki, wawili hao wishirikiana katika bao la tatu.
Bale alimtoka Anaitz Arbilla upande wa kulia kabla ya kumtilia krosi Ronaldo ambaye alifunga bao lake la 13 msimu huu.
Real
Madrid waliongoza kwa 3-0, Ronaldo akifunga la kwanza dakika ya tatu na
la pili dakika ya 48 kabla ya Karim Benzema kufunga la tatu dakika ya
31, lakini wapinzani wao walikuja juu kipindi cha pili na kujpata bao la
kwza dakika ya 53 kwa penalti mfungaji Viera ambaye alifunga tena
dakika ya 55.
Kikosi
cha Real Madrid kilikuwa: Diego Lopez, Carvajal/Arbeloa dk59, Pepe,
Sergio Ramos, Coentrao/Marcelo dk45, Xabi Alonso/Illaramendi dk45,
Modric, Bale, Di Maria, Ronaldo na Benzema.
Rayo Vallecano: Ruben; Tito, Galvez, Arbilla/Larrivey dk51, Nacho; Adrian, Saul; Trashorras, Lass, Falque/Embarba dk69 na Viera.
No comments:
Post a Comment