Goli kipa namba moja wa zamani wa Man United Peter Schmeichel amelaumu na kusema kwamba hakubaliani na kocha wa timu ya Man City Manuel Pellegrini kwa kuchukuwa uwamuzi wa kumuacha benchi kipa namba moja wa timu hiyo Joe Hart eti kwa sababu ameshuka kiwamgo.
Kipa huyo amemuelezea Hart kwamba sio kosa lake kufungwa bali kufungwa kwake kunategemea na uwezo wa safu ya ulinzi wa timu.
Hart amekaa benchi tangu aliposababisha timu yake kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Chelsea na tangu hapo amekuwa akikaa nje na nafasi yake kurithiwa na kipa namba mbili Costel Pantilimon.
Kipa huyo wa zamani aliendelea kusema kwamba katika makosa ya goli kipa yeyote ni vigumu kuamua nani aliyesababisha bali ni kujua ni jinsi gani kosa lilipotokea na kwani safu ya ulinzi wa timu hiyo haijakaa vizuri hasa kwa mchezo mkubwa kama ule.
Vilevile amesema kwamba Hart hakustahili adhabu hiyo kwa kuwa ni kipa mzuri mwenye kiwango cha dunia na kila timu inahitaji huduma yake na kukaa nje kwake kunamsababishia kutojiamini kwa michezo ijayo pindi akipangwa
No comments:
Post a Comment