SULEIMAN
Abdallah Matola sasa anakuwa Kaimu Kocha wa Simba SC baada ya makocha
wote, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ na Msaidizi wake
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kusimamishwa.
Matola ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Simba B, atakuwa Kocha Msaidizi wa kocha mpya waKaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ amewaambia Waandishi wa Habari leo mchana makao makuu ya klabu,
Mtaa wa Msimbazi
kwamba, pamoja na kuwasimamisha makocha hao kwa kutoridhishwa na uwezo
wao, pia wamemsimamisha Mwenyekiti, Alhaj Ismail Aden Rage kwa madai
hawana imani naye.
Kinesi alisema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika jana Dar es Salaam.
Kinesi amesema sasa yeye ndiye atakaimu Nafasi ya Uenyekiti wa klabu hadi hapo Mkutano Mkuu utakapofanyika.
Ikumbukwe Kinesi alichaguliwa kama Mjumbe tu wa Kamati ya Utendaji na Makamu Mwenyekiti ni nafasi ambayo anakaimu baada ya kujiuzulu kwa Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.
Hata hivyo, Rage hakuwepo kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji jana na Kinesi alipoulizwa alisema kiongozi huyo yupo safarini. kigeni, atakayetambulishwa Desemba 1, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment