KLABU ya Barcelona ilimudu kushinda 4-1 dhidi ya Real Betis licha ya Lionel Messi kuumia mapema.
Messi alipata matatizo wakati akikimbia na mpira dakika ya 18 - majeruhi ya tatu ya mguu wake msimu huu.
Neymar
na Pedro walifunga mabao mawili ndani ya dakika mbili kipindi cha
kwanza na Cesc Fabregas akakamilisha ushindi mnono kwa mabao mawili ya
kipindi cha pili, kabla ya Jorge Molina kuifungia kwa penalti Betis
dakika za majeruhi.
Barcelona imesema kwamba Messi ana matatizo ya misuli na atakwenda kufanyiwa vipimo leo. Mwanasoka huyo bora mara nne wa dunia nafasi yake ilichukuliwa na Andres Iniesta dakika ya 21.
No comments:
Post a Comment