Kocha wa timu ya Manchester city amesema kwamba beki wake kisiki Vicent Kompany bado hajapona na kufikia kurudi uwanjani.
Manuel Pellegrini amesema hayo baada ya mazoezi ya leo na kuwaambia mashabiki wasiwe na wasi kwanai punde atarudi uwanjani na kuitumikia timu hiyo.
Hii imekuja baada ya mashabiki wa timu hiyo kumuombea kupona haraka beki huyo hasa baada ya kuonekana kuna mapungufu makubwa kukosekana na beki huyo kutokana na mchezo wao uliopita wa ligi kuu dhidi ya Chelseana kufungwa kwa mabao 2-1.
Beki huyo aliyapata majeraha hayo katika mchezo wao dhidi ya Everton mwezi uliopita na mashabiki kutia hofu kubwa kwa kusekana kwa beki huyo raia wa Belgium.
No comments:
Post a Comment