Kocha mhispania aliyechukua mikoba ya David Moyes ndani ya Everton Roberto Martinez amezungumzia swala la beki wake wa pembeni kuhusiana na kutimkia kwa kocha wake wa zamani Manchester united.mwezi wa January.
Martinez amesema kwamba itakuwa ni swala la kustaajabisha ikiwa Baines akijiunga na timu hiyo kwa wakati huo ikiwa yeye mwenyewe amesema anafuraha kubakia clabuni hapo.
Awali kocha wa United David Moyes alimjumuisha katika mipango yake beki huyo na hakufanikiwa kumsajili beki huyo raia ya Uingereza mwenye miaka 28 na hatimaye kuambulia saini ya Marouane Fallaini tu.
Kocha huyo aliongeza kusema kwamba Baines anafuraha na timu hiyo na anaimani hataondoka clabuni hapo kwa misimu mingine ijayo.
No comments:
Post a Comment