Monday, November 18, 2013

SIMBA YASAJILI KIUNGO MPYA, MTIBWA SUGAR YABALIKI USAJILI

TIMU ya Mtibwa Sugar imebaliki  aliyekuwa kiungo wao  Awadhi Juma kutua katika kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba.



Awadhi ambaye aliichezea mtibwa Sugar kabla ya kutua Thailand katika klabu ya Criracha FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ametua Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser alisema hawana shida na mchezaji huyo kutua Simba kwani atawasaidia katika mzunguko wa pili pia kwa upande wao walishamalizana nae na ni mchezaji huru.

“Awadhi ni mchezaji mzuri na hakuna shida kutua Simba kwa kuwa ni mchezaji huru alishamaliza mkataba na sisi atawasaidia.

“Tunatarajia kukutana ndani ya wiki hii kujadili ripoti ya kocha, Mecky Maxime kwa ajili ya kuanza mchakato wa usajili wa wachezaji,” alisema Jamal.

No comments:

Post a Comment