TANZANIA
Bara maarufu kama Kilimanjaro Stars imepangwa katika Kundi B kwenye
michuano ya CECAFA Challenge pamoja na Zambia, Burundi na Somalia.
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 27 mjini Nairobi, Kenya, wenyeji Harambee Stars wamepangwa na Ethiopia, Zanzibar na Sudan Kusini katika Kundi A.
Mabingwa watetezi, Uganda wamepangwa Kundi C pamoja na Rwanda, Sudan na Eritrea. Ratiba ya michuano hiyo inatarajiwa kutolewa wiki ijayo.
MAKUNDI CHALLENGE 2013:
KUNDI A
Kenya
Ethiopia
Zanzibar
South Sudan
KUNDI B
Tanzania
Zambia
Burundi
Somalia
KUNDI C
Uganda
Rwanda
Sudan
Eritrea.
No comments:
Post a Comment