MECHI
ya kwanza ya Raundi ya michuano ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kwa
wanawake chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini
iliyokuwa ichezwe Mwanza sasa itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Baada
ya ukaguzi uliofanywa na maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
imebainika uwanja huo unatakiwa ufanyiwe marekebisho ambayo hayawezi
kuwahi Desemba 7 mwaka huu, siku ambayo ndiyo mechi hiyo inatakiwa
kuchezwa.
Vyumba vya wachezaji vya Uwanja huo ndilo eneo ambalo linatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa.
No comments:
Post a Comment