Michuano
ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa
klabu za Ligi Kuu inaanza kutimua vumbi Novemba 17 mwaka huu katika viwanja vya
Karume na Azam Complex, Dar es Salaam.
Droo
ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Maji Uhai imefanyika leo (Novemba 8 mwaka
huu) mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) ambapo timu zimepangwa katika makundi matatu.
Kundi
A linaundwa na timu za Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Mbeya City na
Yanga, wakati kundi B ni Ashanti United, Mgambo Shooting, Oljoro JKT na Ruvu
Shooting. Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Rhino Rangers na Tanzania Prisons ndizo
zinazounda kundi C.
Mechi
za ufunguzi kundi A Novemba 17 mwaka huu ni kati ya Azam na Coastal Union (saa
2 asubuhi- Karume), Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Karume). Kundi B ni Ruvu
Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi- Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10
jioni- Karume).
Kagera
Sugar na Mtibwa Sugar (saa 2 asubuhi- Azam) na Rhino Rangers na Tanzania
Prisons (saa 10 jioni- Azam) ndizo zitakazocheza mechi za ufunguzi Novemba 17
mwaka huu katika kundi C.
Robo
fainali ya michuano hiyo itachezwa Novemba 24 na 25 mwaka huu wakati nusu
fainali itapigwa Novemba 26 na 27 mwaka huu. Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu
na ile ya fainali zitachezwa Novemba 30 mwaka.
No comments:
Post a Comment