Wednesday, November 27, 2013

ZANZIBAR YAANZA VIZURI MICHUANO YA CHALLENGE, YAICHAPA SUDAN KUSINI 2-1

ZANZIBAR imeanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuifuga mabao 2-1 Sudan Kusini katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A, Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

Mabao ya Zanzibar Heroes leo yalfungwa na kiungo wa Coastal Union ya Tanga, Suleiman Kassim ‘Selembe’ dakika ya saba baada ya kuipangua ngome ya Sudan Kusini na kufumua shuti lililomshinda kipa Juma Jinaro na Adeyoum Saleh Ahmed dakika ya 67.

Bao la Sudan Kusini lilifungwa na Fabiano Lako dakika ya 73, zikiwa ni dakika tano aiingie kuchukua nafasi ya Francis Khamis.

Zanzibar ingeweza kuondoka na ushindi mnene leo kama washambuliaji wake, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Ally Badru wangetumia vyema nafasi nzuri walizopata. Nafasi nzuri zaidi ambayo Zanzibar walipata ilikuwa dakika ya 43 baada ya Badru kumlamba chenga kipa, lakini Khamis Mcha alipopiga pira ukagonga mwamba na kipa akaudaka.

Zanzibar; Abdallah Rashid, Salum Khamis/Ally Khan dk78, Waziri Salum, Shaffi Hassan, Mohamed Fakhi, Sabri Ali, Masoud Ali, Suleiman Kassim, Awadh Juma na Khamis Mcha/Amour Omar dk44/Adeyoum Saleh dk62. 

Sudan Kusini; Juma Jinaro, Atar Thomas, Philip Delfino, Edomon Amadeo, Richard Justin, Wiiam Offiri, Jimmy Erasto, Thomas Jacob, Godfrey Peter, Francis Khamis/Fabiano Lako dk68 na James Joseph.

No comments:

Post a Comment