KOCHA
David Moyes na kikosi chake cha Manchester United walipatwa na mshituko
wakiwa angani Ujerumani jana kwa safari ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa
Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen baada ya ndege hiyo kughairi kutua
Uwanja wa Ndege wa Cologne.
Ndege
ya United ilikuwa umbali wa mita 400 kuelekea chini Uwanja wa Ndege wa
Cologne wakati Rubani alipofoka akisema kuna ndege nyingine katika eneo
alilotaka kutua.
Wakati
wachezaji wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England wakirejea kwenye siti
zao, Rubani akalazimika kuzunguka upande mwingine kuishusha ndege hiyo
Wametulia: Ashley Young na Jonny Evans wakiwa Uwanja wa ndege wa Manchester kabla ya safari ya Ujerumani
Rio Ferdinand ametweet juu ya kutua kwao salama
David Moyes na Wayne Rooney Uwanja wa Ndege wa Manchester
Kikosi
kizima cha United, wakiwemo wachezaji, kocha David Moyes na viongozi
wote wa benchi la Ufundi walikuwa kwenye ndege na beki Rio Ferdinand akatweet baada ya kutua: "Tumetua Ujerumani...baada ya kupatwa msukosuko hivi wakati wa kutua.’
Sir
Bobby Charlton, ambaye alikuwepo katika msafara wa United uliopata
ajali mjini Munich mwaka 1958, na Sir Alex Ferguson hawakuwamo kwenye
ndege hiyo
David Moyes alikuwa mwenye furaha kiasi cha kutosha baada ya kutua Ujerumani wakati anazungumza na Wandishi wa Habari
Chris Smalling alikuwa kwenye hali nzuri pia
No comments:
Post a Comment