Thursday, December 12, 2013

BAUSI NA HSIRA ZAKE ZA MKIZI

Wakati leo michuano ya afrika mashariki na kati umaarufu kama chalenji ikiwa ndio inaingia siku yake ya fainali ikizikutnisha kenya na sudan, kuna maoni mbalimbali kutoka kwa wadau wa soka ndani na nje ya nchi wengi wao wakionekana kufurahishwa na michuano hiyo jinsi ilivyokuwa ikiendelea lakini kwa upande wa wa zanzibari na watanzania waliowengi wanaendelea kushangazwa na hatua iliyochukuliwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya zanzibar kuwaacha wachezaji ambao wenye uzoefu na michuano ya kimataifa na kuwachukua wachezaji ambao hawana uzoefu jambo ambalo limepelekea timu hiyo kutolewa katika hatua ya awali na kushindwa kusonga mbele katika hatua za mtoano jambo ambalo limewakasirisha sana wadau wa soka visiwani zanzibar kwa vile timu ya zanzibar heroes ni moja ya timu zinazotowa upinzani na zinaogopewa katika michuano ya chalenji lakini kutokana na hatuwa iliyochukuliwa na bausi ambayo imetafsiriwa kuwa ni hasira na kuwakomoa wachezaji hao ambao wengi wao wanacheza ligi ya tanzania bara katika michuano ya mwaka huu timu ya taifa ya zanzibar(zanzibar heroes) imeonekana kuwa mbwambwa kwa kumaliza michuano hatua ya makundi na kupata pointi 3 ilizozipata kutoka kwa kibonde sudani kusini na kushindwa kufurukuta mbele ya Ethiopia na wenyeji Kenya na kutupwa nje ya michuano kwa aibu.

MAONI YANGU JUU YA HATUA YA  BAUSI
kama mdau na mpenzi wa soka na mzalendo wa soka la zanzibar nilifuatilia kwa makini uteuzi wa kikosi cha zanzibar heroes kilichokwenda kwenye michuano ya chalenji lakini nilisikitishwa sana na kikosi alichokiteuwa ambacho kwa upande wangu kabla hata ya kuondoka nilikuwa sina imani nacho na niliamini kuwa kitakuwa ni gari la pointi kwa timu pinzani
Bausi baada ya kuteuwa kikosi chake ambacho aliwaacha wachezaji wazoefu kama nadir haroub (cannavaro),aggrey morris (chacha), nassor masoud chollo, Abdi kassim (babi), Abdoulhalim humud kabla ya kumtema kipa mzoefu wa Azam fc Mwadini Ally (reina) siku chache kabla ya kuelekea nairobi kenya .

Akitaja sababu za kuwatema wachezaji hao Baausi alisema kuwa hawana nidhamu na kusisitiza kuwa mchezaji asiye na nidhamu hana nafasi katika kikosi chake, Sababu nyengine alisema kuwa ni kuwapa nafasi vijana,ni kweli wachezaji hawana nidhamu?

kabla ya kujibu swali hili tuangalie historia na sifa (cv) za wachezaji hawa

Nadir haroub: nadir anajulikana na wengi kwa jina la cannavaro ni kijana aliyekulia katika mazingira ya soka tangu udogboni huku watu kama hassan haji hamza (chura),na selemani (kisheta) wakiwa ni chachu ya mafanikio ya cannavaro vilevile bidii ucheshi na nidhamu ndani na nje ya uwanja

 

No comments:

Post a Comment