Thursday, December 12, 2013

IVO MAPUNDA ATUA SIMBA RASMI,ALA MKATA BA WA MWAKA MMOJA NA NUSULA MKATA

KIPA namba moja wa Tanzania, Ivo Philip Mapunda, usiku huu amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu kujiunga na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Ivo anasaini Simba SC, baada ya kung’ara akiwa na kikosi cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka huu.

 Ivo aliiongoza Kilimanjaro Stars kufika Nusu Fainali ya Challenge baada ya kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi Uganda ‘The Cranes’ kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90, kipa huyo akicheza mikwaju miwili.  Akizungumza  baada ya kusaini Simba SC, Ivo alisema kwamba ameamua kusaini timu hiyo Mtaa wa Msimbazi baada ya kuridhishwa na maslahi aliyopewa.

Ivo alisema kwamba Simba SC ni timu kubwa na anaamini atafanya vizuri.     “Sina wasiwasi, mimi ni kipa mzoefu na hata Watanzania wanajua uwezo wangu, baada ya kusaini, sasa ni kazi tu, kikubwa naomba ushirikiano na benchi la Ufundi, uongozi, wachezaji wenzangu na mashabiki na wadau kwa ujumla, ”alisema Ivo aliyewahi kudakia Yanga SC.
  Ivo Philip Mapunda alizaliwa Novemba 14, mwaka 1979 na kisoka aliibukia katika klabu ya Tukuyu Stars kabla ya kuhama Prisons zote za Mbeya, baadaye Moro United mwaka 2005 kabla ya kutua Yanga msimu uliofuata, 2006. Aliidakia Yanga hadi 2009 akahamia St George ya Ethiopia alikopiga kazi msimu mmoja, akarejea nyumbani kuidakia African Lyon 2011 kabla ya 2012 kuhamia Bandari ya Mombasa, Kenya ambako alifanya kazi kwa miezi sita akasajiliwa na Gor Mahia.

Ivo anamaliza Mkataba wake Gor Mahia Desemba 16, mwaka huu na ataidakia kwa mara ya mwisho klabu hiyo katika mechi ya Kombe la DSTV Desemba 14 dhidi ya Tusker FC na baada ya hapo atapakia kila kilicho chake na kuja kuanza maisha mapya Msimbazi.

No comments:

Post a Comment