MABAO
ya Fernando Torres dakika ya 16 na Ramires dakika ya 35 yameipa ushindi
wa 2-1 Chelsea dhidi ya Crystal Palace jioni ya leo Uwanja wa Stamford
Bridge katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Bao pekee la Crystal lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Chamakh dakika ya 29.
Ushindi
huo unamaanisha Chelsea inaweza kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya
England ikiifunga Arsenal Desemba 23 Uwanja wa Emirates.
Katika
mechi nyingine za Ligi hiyo leo, Manchester City imeifunga 6-3 Arsenal,
Cardiff City imeilaza 1-0 West Bromwich, Everton imeikung'uta 4-1
Fulham, Newcastle United imetoka 1-1 na Southampton, West Ham United
imetoka 0-0 na Sunderland sawa na Hull City na Stoke City.
No comments:
Post a Comment