Tuesday, December 24, 2013

FELLAINI AFANYIWA PASUAJI WA MKONO

Mcheza kiungo wa Manchester United Marouane Fellaini huenda asicheza mechi yoyote kwa muda wa wiki sita zijazo baada ya kufanyiwa upasuaji wa mkono.

Fellaini, 26, amekuwa akiuguza jeraha la mgongo na wasimamizi wa Manchester United wakaamua mchezaji huyo ambaye pia alikuwa na jeraha lingine, afanyiwa upasuaji wa mkono kwanza.

Fellaini amekuwa na tatizo hilo la mkono tangu alipojeruhiwa wakati wa mechi yao ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk Oktoba mwaka huu.

Fellaini alipata jeraha lingine la mgongo wakati wa mechi ya ligi kuu dhidi ya Everton tarehe nne Desemba.
Moyes ambaye alimsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 27.5 Septemba mwaka huu, amesema kuwa tatizo hilo la mgongo huenda likachukua muda mrefu zaidi.

No comments:

Post a Comment