WASHINDANI
10 wa tuzo ya Mwanamichezo Bora Chipukizi wa mwaka wa Shirika la
Utangazaji Uingereza (BBC) 2013 wametajwa akiwemo kinda wa Manchester
United, Adnan Januzaj.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 18 atatarajia kufuata nyayo za mchezaji
mwenzake, Wayne Rooney, ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka 2002.
Januzaj
alizaliwa Ubelgiji lakini bado hajaamua ataichezea nchi gani na kwa
sasa hawezi kuchezea England. Pamoja na kwamba si Muingereza, anastahili
tuzo ya BBC kwa kuwa ni raia na anacheza Uingereza na mafanikio yake
ameyapata katika nchi hii si timu ya taifa.
Mafanikio mapema: Adnan Januzaj ameingia kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya Mwanamichezo Bora wa BBC
Januzaj
atachuana na Dina Asher-Smith, akiwa na umri wa miaka 17 ameweka rekodi
ya kuwa binti mdogo wa pili kushinda Medali katika mashindano ya Riadha
ya Dunia, alipoisaidia timu ya wanawake ya Uingereza kutwaa Shaba
katika mbio za mita 4x100 relay.
Wengine
kwenye orodha hiyo ni pamoja na Charley Hull, mwenye umri wa miaka 17
aliyekuwa kinda zaidi kucheza michuano ya gofu ya Ulaya au Marekani,
Kombe la Solheim, akifunga pointi mbili kati ya tatu Ulaya ikitamba kwa
mara ya kwanza katika ardhi ya Amerika.
Mvunja
rekodi mwingine kwenye orodha ni Amber Hill, ambaye alikuwa ana umri wa
miaka 15 tu wakati alipoibuka mshindi kinda zaidi daima katika mchuano
ya kombe la Dunia ya wakubwa na kumaliza msimu akishika nafasi ya tano
katika ubora duniani.
Dina Asher-Smith (kulia) pia yumo
WASHINDI WA AWALI
2012: Josef Craig
2011: Lauren Taylor
2010: Tom Daley
2009: Tom Daley
2008: Ellie Simmonds
2007: Tom Daley
2005: Harry Aikines-Aryeetey
2006: Theo Walcott
2004: Andy Murray
2003: Kate Haywood
2002: Wayne Rooney
2001: Amy Spencer
2011: Lauren Taylor
2010: Tom Daley
2009: Tom Daley
2008: Ellie Simmonds
2007: Tom Daley
2005: Harry Aikines-Aryeetey
2006: Theo Walcott
2004: Andy Murray
2003: Kate Haywood
2002: Wayne Rooney
2001: Amy Spencer
Wengine
ni muogeleaji James Guy, bti kinda kushindana kwa Uingereza katika
michuano ya mmoja mmoja; Jess Judd, mwanariadhakinda kuiwakilisha
Uingereza katika mbio za mita 800 katika mashindano ya dunia; muogeleaji
wa mashindano ya walemavu, Amy Marren ambaye akiwa na umri wa miaka 15
alifanikiwa kushinda Medali nne za Dhahabu katika michuano ya mwaka 2013
ya IPC ya ubingwa wa dunia; Bingwa kinda wa Ulaya wa kunyanyua uzito,
Rebekah Tiler; mkimbiaji mlemavu, Isaac Towers, ambaye akiwa na umri wa
miaka 15, alivunja rekodi ya wakubwa Ulaya ya mita 1500; Kimberley Woods
ambaye alishinda mataji kadhaa mwaka 2013 yakiwemo ya Dhahabu katika
C1W Kombe la Dunia la wakubwa.
Tuzo
ya Mwanamichezo Chipukizi wa mwaka wa BBC, inatolewa kwa kinda
aliyefanya vizuri kwa mwaka husika, ambaye ana umri usiozidi miaka 17 na
baadhi ya waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni pamoja na Ellie Simmonds, Wayne
Rooney, Tom Daley na Andy Murray.
Moscow:
Dina Asher-Smith (wa pili jykua) aliweka ekodi ya kuwa binti kinda wa
kwanza kutwaa Medali ya Shaba katika mbio za mita 4x100.
No comments:
Post a Comment