Tuesday, December 3, 2013

MCHEZO KATI YA KILI STARS NA BURUNDI HATARINI KUFANYIKA

Timu ya taifa ya Burundi imezuiliwa kwenye hotel waliyofikia kutokana na kushindwa kulipa gharama za pango huko nchini walipo wanaposhiriki michuano ya Cecafa Senior Challenge Cup.

Timu hiyo ya Burundi inacheza na Kilimanjaro Stars kesho Jumatano huko Nakuru lakini jioni ya leo wamefungiwa kwenye htel ya Milele Hotel iliyopo eneo la South ‘C’ baada ya wamiliki kukataa kuwaruhusu kutoka kwenda Nakuru mpaka bili zitakapolipwa.

"Wakati timu nyingine zikisafiri kwenda Nakuru, Burundi bado wamefungiwa kwenye vyumba vyao baada ya utawala kukataa kuwaruhusu," kilisema chanzo cha habari.

Chanzo hicho cha habari kimesema kwamba waandaji hawajachukua hatua yoyote kutafuta muafaka wa suala hilo. Jumapili, shirikisho la soka la Kenya kupitia raisi wake Sam Nyamweya alisema kwenye mahojiano na kitu kimoja cha radio kwamba wanakabiliwa na ukata mkubwa.

No comments:

Post a Comment