KLABU
ya Manchester United imeonywa kwamba mchezaji chaguo la kwanza la David
Moyes katika usajili wa dirisha dogo, Marco Reus atawagharimu hadi
Pauni Milioni 40 ili kumpata.
Kiungo Reus ana thamani ya Pauni Milioni 29.4 Borussia Dortmund.
Lakini inafahamika mambo yamebadilika tangu Bayern Munich ionyeshe nia ya kutaka kumsajili Mario Gotze.
Itakugharimu!
Borussia Dortmund inataka dau la Pauni Milioni 40 ili kumuuza Marco
Reus, ambaye anatakiwa na Manchester United katika usajili wa Januari
Kiwango
cha dunia: United itavunja rekodi ya dau la usajili kumsajili mchezaji
mwenye kipaji, Reus, ambaye kocha David Moyes amemtambulisha kama chaguo
la kwanza katika wachezaji anaowataka
Mabingwa
hao wa Ligi Kuu ya England watatakiwa kuvunja rekodi yao ya dau la
usajili ili kuipata saini ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.
Wasaka vipaji wa United wakuwa wakisaka mchezaji wa kiwango cha dunia kwa nafasi yoyote.
Pamoja
na hayo, kiungo huyo anabakia kuwa chaguo lao la kwanza, ingawa pia
wanasaka na washambuliaji, beki wa kushoto na beki wa kati waje kuwa
warithi wa Patrice Evra na Rio Ferdinand mwishoni mwa msimu.
Anaelekea mwisho? United imeanza kusaka mbadala wa Patrice Evra
No comments:
Post a Comment