KOCHA David Moyes ameendelea kupambana
baada ya jana kuiongoza Manchester United kushinda mabao 2-0 dhidi ya
Stoke City katika Kombe la Ligi England.
Ushindi huo wa United jana ulitokana na mabao ya Ashley Young dakika ya 61 na Patrice Evra dakika ya 78.
Raha ya bao: Ashley Young (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Manchester United bao la kwanza dhidi ya Stoke City
Katika mchezo mwingine, mshambuliaji Emmanuel Adebayor alirejea uwanjani na kufunga bao moja wakati timu yake, Tottenham Hotspur ikifungwa 2-1 na West Ham United, mabao ya Jarvis dakika ya 80 na Maiga dakika ya 85. Man United sasa itamenyana na Sunderland katika Nusu Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Capital One, wakati West Ham itakipiga na Manchester City.
Adebayor akishangilia bao lake ambalo hata hivyo halikuweza kuinusuru Spurs na kipigo |
Nayo Manchester City iliifunga 3-1 Leicester na kufikisha jumla ya mabao 75 katika mechi 25 za mashindano yote msimu huu.
Free-scoring: Sergio Aguero (centre) and Alvaro Negredo (left) are combining effectively in Manchester
|
No comments:
Post a Comment