MARA
tu baada ya kutolewa katika Klabu Bingwa ya Dunia a FIFA, wazi
Ronaldinho alitaka kurejea chumba cha kubadilishia nguo cha Atletico
Mineiro kujiliwaza.
Lakini
alilazimika kubaki uwanjani baada ya kuvamiwa na wachezaji wa Raja
Casablanca, waliomsalimia na kumuomba viatu vyake vya Nike!
Timu
hiyo Morocco iliendeleza wimbi lake la ushindi nyumbani kwa ushindi wa
mabao 3-1, wakimtoa nishai Mbrazil huyo ambaye alifunga bao zuri la
mpira wa adhabu- katika jitihada zake za kushinda taji hilo kwa mara ya
kwanza tangu alipofika fainali akiwa na Barcelona mwaka 2006.
Mwenye bahati yake: Vivien Mabide akiwa ameshika moja ya viatu hivyo baada ya mechi
Wachezaji wa Casablanca
Mouchine
aliifungia Raja bao la kwanza kabla ya Ronaldinho kusawazisha. Lakini
Raja ikapata bao la pili dakika ya 84 kwa penalti na Vivien Madibe
akahitimisha ushindi huo dakika ya mwisho kwa bao la tatu.
Timu hiyo ya Morocco sasa itamenyana na mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich Jumamosi katika Fainali mjini Marakech.
Wachezaji wa Raja Casablanca wakisherehekeas baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Atletico Mineiro Uwanja wa Marrakech
Ronaldinho akiwa haamini macho yake na chini akishangilia baada ya kufunga
No comments:
Post a Comment