NYOTA
wa Brazil, Neymar jana alianza kutanua mbawa zake Ulaya, baada ya
kufunga mabao matatu ndani ya dakika 13 katika ushindi wa Barcelona ya
Hispania wa 6-1 dhidi ya Celtic ya Scotland katika mchezo wa mwisho wa
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa
kufanya hivyo, Neymar ameingia kwenye orodha ya wachezaji waliofunga
hat trick za haraka, yaani kufunga mabao matatu ndani ya muda mfupi
katika michuano ya Ulaya.
Mungu niwezeshe zaidi; Neymar akimshukuru Mungu baada ya kukamilisjha hat trick ndani ya dakika 13 jana
|
Neymar akishangilia hat trick yake ya ndani ya dakika 13
Desemba
7, 2011 Bafetimbi Gomis wa Lyon aliweka rekodi ya hat trick ya mapema
zaidi dhidi ya Dinamo Zagreb ndani ya dakika saba, akivunja rekodi ya
Mike Newell wa Blackburn aliyetumia dakika tisa na Marco van Basten wa
AC Milan aliyetumia dakika 11.
Desemba 7, mwaka jana Claudio Pizarro wa
Bayern Munich naye aliingia katika orodha ya wachezaji waliofunga hat
trick za mapema, akifunga mabao matatu dhidi ya Lille ya Ufaransa ndani
ya dakika 15.
Barcelona
jana licha ya kuwakosa Andres Iniesta aliyebaki benchi, Leo Messi
ambaye bado majeruhi na Cesc Fabregas anayetumikia adhabu, iliichapa
mabao 6-1 Celtic.
Neymar
aliyeongoza safu ya ushambuliaji hakufanya makosa baada ya kufunga hat
trick yake ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa dakika za 45, 48 na 58,
wakati mabao mengine yalifungwa na Pique dakika ya saba, Pedro dakika ya
39, na Tello dakika ya 72.
Je,
huu ni mwanzo wa Mbrazil huyo kuwasha moto zaidi Ulaya kuelekea kuwa
mfalme wa dunia, akiwapindua Ronaldo na Messi? Bila shaka hilo ni jambo
la kusubiri na kuona.
HAT-TRICKS ZA MAPEMA ZAIDI LIGI YA MABINGWA
Tarahe | Mchezaji | Timu yake | Mpinz | Minutes |
07/12/2011 | Bafetimbi Gomis | Lyon | Dinamo Zagreb | 7 |
06/12/1995 | Mike Newell | Blackburn | Rosenborg | 9 |
25/11/1992 | Marco van Basten | AC Milan | IFK Gothenburg | 11 |
11/12/2013 | Neymar | Barcelona | Celtic | 13 |
07/12/2012 | Claudio Pizarro | Bayern Munich | Lille |
No comments:
Post a Comment