BAO
la Ndahinduka Michel dakika ya 75 limeipa Rwanda ushindi wa 1-0 dhidi
ya Eritrea katika mchezo wa mwisho wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya
Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge leo Uwanja wa Kenyatta,
Machakos, Kenya.
Kwa ushindi huo, Rwanda inafanikiwa kufuzu Robo Fainali kama best loser wa pili, baada ya Burundi na sasa Nahodha wa timu hiyo, kiungo Haruna Niyonzima anayechezewa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam anaendelea kula maisha Kenya.
Zanzibar
imeaga mashidano pamoja na Eritrea, Sudan Kusini na Somalia na sasa
Amavubi inaungana na Tanzania Bara, Uganda, Kenya, Sudan, Ethiopia na
Zambia kwenda Mombasa katika Nane Bora.
Kenya imeshinda kura ya sarafu na kuwa kinara wa Kundi A, baada ya kulingana kwa kila kitu na Ethiopia.
No comments:
Post a Comment