MSHAMBULIAJI Luis Suarez amethibitisha hataondoka Liverpool katika dirisha dogo— na amesema Ligi Kuu England ni bora duniani.
Lakini bado anagoma kuongeza Mkataba na klabu hiyo ya Anfield.
Real
Madrid imekuwa ikihusishwa na kumnunua mchezaji huyo wa Uruguay ifikapo
January ili akakate kiu yake ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
Mtambo wa mabao: Suarez alifunga mabao manne Liverpool ikishinda dhidi ya Norwich jana usiku
Lakini
bada ya kufunga mabao manne kattika ushindi dhidi ya Norwich jana
aliliambia gazeti la Marca: "Ninapokuwa nina furaha nje ya Uwanja;
inaonyeshwa na kiwango changu uwanjani. Nina furaha katika Ligi Kuu ya
England; ni ambako kuna ligi bora,".
Alipoulizwa kama atabaki hadi mwishoni mwa msimu unaoendelea, alisema: "Ndiyo, nina furaha hapa na nitabaki,".
Suarez
sasa anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu ya England, akiwa amefunga
mara 13 licha ya kukosa mechi tano za mwanzo akitumikia adhabu.
"Bahati
nzuri nafunga mabao kufidia mechi nilizokosa. Ninapata hali ya
kujiamini kuweza kuisaidia zaidi timu. Kitu cha msingi ni kufuzu Ligi ya
Mabingwa baada ya muda mrefu ya kuwa nje ya nne bora. Nataka kuisaidia timu kufikia mafanikio hayo,".
Licha
ya kuonyesha kiwango cha juu, mshambuliaji huyo wa Liverpool amesema
kwamba anabaki kuwa chini ya Leo Messi na Cristiano Ronaldo.
Alipoulizwa
kuhusu tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, alisema: "Ballon d’Or
ni haiwezekani kwangu, nyota wengine wakiwania tuzo hiyo. Wako katika
kiwango kingine,".
Wakali: Suarez amesema hana ubora wa kushinda Ballon d'Or mbele ya Cristiano Ronaldo au Leo Mess
No comments:
Post a Comment