KAIMU
Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Decolas
Kiiza, amesema kwamba Shikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeridhia
mshambuliaji Emmanuel Arnold Okwi kujiunga na mabingwa wa Tanzania,
Yanga SC.
“Ndiyo,
tuliwaandikia FIFA na wamesema mchezaji huyo alikuwa huru kusajiliwa,”
Kiiza aliiuambia mtandao wa soka, MTNFootball.com.
Mapema wiki hii, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FUFA na kiungo wa zamani wa SC Villa ya Uganda na timu ya taifa ‘The Cranes’, Edgar Watson, alisema waliwasiliana na FIFA kupata ufafanuzi zaidi juu ya suala la Okwi kusajiliwa Yanga.

Okwi
amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es
Salaam jioni ya leo tayari kuanza kuutumikia Mkataba wake wa miaka
miwili ndani ya klabu ya Yanga SC ya Tanzania.
Okwi
alitua kwa ndege ya RwandaAir Saa 9:55 jioni na kulakiwa na viongozi na
wapenzi kadhaa wa timu hiyo JNIA kabla ya kupakiwa kwenye gari ndogo
aina ya saluni alilokuwa akiendesha Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano
ya Kimataifa ya Yanga, Seif Ahmed ‘Magari’ na kuondoka. Alikaa kiti cha
nyuma na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro.
Okwi
alitokea geti la wageni maalum la JNIA na kusindikizwa na Polisi huku,
umati wa mashabiki wa Yanga ukimshangilia na kumfanya atoke kwa taabu
hadi kupanda gari.
Mara
tu baada ya kutoka nje ya JNIA, Okwi alisema; “Nimekuja Yanga kufanya
kazi,” na alipoulizwa kuhusu utata wa usajili wake, akasema; “Mimi
nimekuja kufanya kazi, hayo mengine, mamlaka husika zitajua,”alisema
Okwi aliyekuwa amevalia jezi nambari 25 ya Yanga.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdaollah
Ahmed Bin Kleb alisema kwamba mchezaji huyo anakwenda moja kwa moja
kambini, Protea Hotel kuungana na wenzake tayari kwa mchezo wa Jumamosi
wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu, Simba SC.
Simba
na Yanga zitamenyana Jumamosi katika mchezo ambao iwapo dakika 90
zitamalizika kwa sare, mikwaju ya penalti itaamua mshindi.
Mchezo huo, unaoandaliwa na wadhamini wa klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager, unatarajiwa kuchezeshwa na refa Ramadhan Ibada ‘Kibo’ kutoka Zanzibar, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba na Simon Charles kutoka Dodoma, wakati refa wa akiba atakuwa Israel Nkongo wa Dar es Salaam na mtathimini wa waamuzi ni Soud Abdi wa Arusha. Jumapili Yanga SC ya Dar es Salaam ilitangaza kumsajili Okwi raia wa Uganda kwa Mkataba wa miaka miwili na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Abdallah Ahmed Bin Kleb alisema Okwi ataanza kuichezea timu hiyo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na michuano ya Afrika. Etoile du Sahel ya Tunisia ilimnunua Okwi kutoka Simba SC Januari mwaka huu kwa dola za Kimarekani 300,000, lakini mchezaji huyo akaamua kuachana na klabu hiyo na kurejea kupumzika kwao Uganda, kwa madai hakulipwa mishahara kwa miezi mitatu.

Wakati
huo huo, Etoile hadi sasa haijailipa Simba SC fedha zake za kumnunua
mchezaji huyo na sakata lake limefikishwa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA).
Baada
ya Okwi kukaa bila kucheza kwa miezi sita, Shirikisho la Soka la Uganda
(FUFA) lilimpigania aruhusiwe kurejea nyumbani kuichezea SC Villa ya
huko ili kunusuru kiwango chake.
Hata
hivyo, baada ya kung’ara na timu ya taifa ya Uganda ‘The Ceanes’ nchini
Kenya kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Challenge mwezi huu, Okwi amesajiliwa Yanga SC.
Bin
Kleb alisema kwamba walimsajili Okwi tarkiban siku sita zilizopita,
lakini Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ilipatikana Jumapili na
ndiyo maana wakaamua kumtangaza.
Alipoulizwa
kuhusu utata wa sakata lake ambalo limefika hadi FIFA, Kleb alisema;
“Tumefuatilia kote, hadi kwa wanasheria, na tumefanikiwa kupata hadi ITC
yake, nawaambia mashabiki wa Yanga wajue viongozi wao wanafanya kazi,
hatuna stori nyingi, sisi tunafanya vitendo, tunafanya kazi kwa siri
sana,”.
“Na
tumepitia sehemu zote, tumeona kabisa tuko sahihi katika kumsajili
mchezaji huyu na hakutakuwa na tatizo lolote upande wetu,”alisema.
Lakini
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe
amesema kwamba watani wao wa jadi, Yanga SC wameingia mkenge kumsajili
Okwi na labda watamtumia kwenye mchezo wa Nani Mtani Jembe pekee, lakini
zaidi ya hapo hatacheza Jangwani kwenye michuano yoyote rasmi.
Kapteni
huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), alisema kwamba
Okwi ni mchezaji halali wa Etoile du Sahel ya Tunisia na hawezi kucheza
Yanga.
“Mimi
sina wasiwasi, naangalia tu sarakasi zao nikiwa najua wataangukia wapi.
Yule mchezaji Yanga wameingizwa mkenge na FUFA (Shirikisho la Soka
Uganda). Kwa sababu, Etoile ilimtoa kwa mkopo SC Villa na ndiyo maana
hata FUFA walipotaka kumtumia katika CHAN, wakaambiwa haiwezekani kwa
kuwa yule ni mchezaji wa Etoile,”alisema Hans Poppe.
No comments:
Post a Comment