ROBO
Fainali za kwanza za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Chalenge zinatarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Manispaa, Mombasa,
Kenya.
Mechi
inayotarajiwa kuteka hisia za wengi ni kati ya mabingwa watetezi,
Uganda The Cranes dhidi ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars itakayoanza
saa 8:00 mchana, ingawa kutakuwa na mchezo mwingine kati ya Kenya na
Rwanda saa 10:00 jioni.
REKODI YA BARA NA UGANDA CHELLENGE TANGU 1973…
Sept. 29, 1973;
Uganda 2-1 Tanzania, Fainali
Sept. 25, 1974
Tanzania 1-1 Uganda(Bara ilishinda penalti 5-3 fainali)
Nov. 9, 1979
Tanzania 5 – 3 Uganda Kundi A
Nov. 17, 1982
Uganda 1 – 0 Tanzania Kundi A
Des. 1, 1984
Uganda 1 – 1 Tanzania Kundi A
Des. 8, 1989
Uganda 5 – 1 Tanzania Kundi A
Des. 17, 1990
Uganda 1-1 Tanzania (Uganda ilishinda penalti 6-5 Nusu Fainali)
Nov. 30, 1991
Uganda 5 – 0 Tanzania Kundi A
Nov. 28, 1992
Uganda 1 – 0 Tanzania B ‘Kakakuona’, Fainali
Des. 10, 1994
Tanzania 2-2 Uganda (Bara ilishinda penalti 4-3 fainali) Nov. 22, 1996
Uganda 1 – 0 Tanzania Kundi A
Des. 11, 2001
Tanzania 1 - 0 Uganda Kundi B
JanuarI 9, 2008
Uganda 2 - 1 Tanzania Kundi A
Nov. 29, 2009
Tanzania 0-2 Uganda Kundi C
Des. 10, 2010
Uganda 0 – 0 Tanzania (Bara ilishinda penalti 5-4 Nusu Fainali
Des. 8, 2011
Uganda 3-1 Tanzania (Nusu Fainali dakika 120)
Des 6, 2012
Tanzania 0–3 Uganda (Nusu Fainali)
Des 7, 2013;
Tanzania Vs Uganda, Nusu Fainali
Stars
wanaingia katika sura ya unyonge kumenyana na The Cranes inayofundishwa
na kocha hodari Afrika, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ kutokana na
kufungwa mfululizo na wapinzani wao hao siku za karibuni.
Timu
ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayoundwa na idadi kubwa ya
wachezaji wa Bara ilifungwa nyumbani na ugenini na Uganda katika mechi
za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za CHAN.
Lakini
pia, Uganda imeonyesha ni tishio katika Challenge ya mwaka huu baada ya
kufuzu Robo Fainali kwa kushinda mechi zake zote za Kundi C, wakati
Bara ilipata ushindi mwembamba wa 1-0 mara mbili na sare moja hivyo
kushika nafasi ya pili Kundi B.
Kocha
Mdenmark, Kim Poulsen amesema kwamba anawaheshimu Uganda ni timu nzuri
na anatarajia mchezo utakuwa mgumu, lakini yeye amewaandaa vyema vijana
wake kushinda mechi ya leo.
Micho
pia amesema Stars ni wazuri hasa baada ya kuwasili kwa washambuliaji wa
TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao amesema
wakiungana na Mrisho Ngassa watetengeneza safu kali ya ushambuliaji.
Kwa ujumla makocha wote wanaogopana kuelekea mchezo huo- jambo ambalo linaashiria hiyo ni mechi isiyotabirika hata chembe.
Kama
alivyosema Micho, safu ya ushambuliaji ya Stars leo inatarajiwa
kuongozwa na Ngassa, Ulimwengu na Samatta wakati viungo wanaweza kuwa
Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Athumani Iddi ‘Chuji’.
Langoni ataanza Ivo Mapunda, kulia Himid Mao, kushoto Erasto Nyoni na katikati Said Morad na Kevin Yondan.
Kwa
upande wa mabingwa watetezi, Uganda, Emanuel Okwi, Hamisi Kiiza na Dani
Sserunkuma wanatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji, wakati wengine
kikosini watakuwa Nico Wadada, Godfrey Kizito, Khalid Aucho, Brian
Majwega, Vincent Kayizzi, Godfrey Walusimbi, Savio Kabugo na Benjamin
Ochan langoni.
Kenya inapewa nafasi kubwa ya kuitoa Rwanda katika mchezo wa pili. Je, Stars itafuta uteja kwa The Cranes leo?
No comments:
Post a Comment