WACHEZAJI wa Manchester United wamezuru katika hospitali mbili jijini humo jana.
Katika
ziara hiyo kwenye hospitali za Royal Manchester Children's Hospital na
The Christie, wachezaji wa timu ya kwanza wakiwemo Michael Carrick,
Marouane Fellaini na Adnan Januzaj waliwatakia watoto heri ya Krisimasi.
Pamoja na hayo, wachezaji hao walioongozana na sanamu la Fred the Red, waliwasilisha zawadi kwa vijana hao na kupiga nao picha.
Ziara: David de Gea (wa pili kushoto), Luis Antonio Valencia (nyuma) na Michael Carrick (kulia) akiwa na shabiki mtoto
Siku maalum: Marouane Fellaini (kushoto) na Adnan Januzaj wakikabidhi zawadi kwa
Shabiki mmoja kinda wa United akionyesha furaha yae kwa Javier Hernandez na Darren Fletcher
Fletcher amesema ni heshima kubwa kutembelea watoto na kuwapa zawadi za Krisimasi
Siku ya kukumbukwa: Carrick, Valencia, De Gea na Ashley Young (kulia) wakiwa na shabiki na mama yake
No comments:
Post a Comment