Friday, January 3, 2014

ASHANTI YAANZA VIBAYA MICHUANO YA MAPINDUZI, YAPIGWA KIMOJA NA TUSKER YA KENYA

ASHANTI United imeanza vibaya michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kufungwa bao 1-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa Kundi C usiku huu, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bao pekee lililoizamisha Ashanti hii leo limefungwa na Joshua Oyoo dakika ya 24, akiunganisha krosi ya Ali Abondo.
Kocha Kibadeni kushoto na wasaidizi wake, Nico Kiondo na Mfaume Athumani katika mechi ya leo Uwanja wa Amaan

Kocha mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ alibadilisha wachezaji wanne kwa mpigo mwanzoni mwa kipindi cha pili, ili kuongeza uhai katika timu yake.
Aliwatoa Anthony Matangalu, Juma Jabu, Faki Hakika na Joseph Mahundi na kuwaingiza Hussein Mkongo, Abdul Mtiro, Paul Maona na Malick Jaffar.
Pamoja na mabadiliko hayo, Ashanti iliyochukua nafasi ya Yanga SC iliyojitoa  kwenye mashindano haya, haikuweza kupata bao la kusawazisha.


Picha kwa msaada wa Binzubeiry blog. 

No comments:

Post a Comment