GWIJI
wa soka kutoka taifa la Ureno, Eusebio amefariki dunia, akiwa na umri
wa miaka 71, baada ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo kwa muda mrefu.
Eusebio
alizaliwa nchini Msumbiji kama Eusebio da Silva Ferreira na anatajwa
kama mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani.
Aliitumikia
klabu ya mjini Lisbon,Benfica FC kwa miaka 22 ambapo uwezo wake wa mbio
na kasi, kuutumia vyema mguu wake wa kulia na mbinu za kimpira kulimpa
umaarufu sana nchini Ureno na kubatizwa jina la The Black Pearl or the
Black Panther.
Wakati
wa uchezaji wake alifunga mabao 733 katika mechi 745, pia alifunga
mabao tisa kwenye michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1966 na kuwa
mfungaji bora wa mashindano hayo na kuisaidia Ureno kushika nafasi ya
tatu kwenye michuano hiyo.
Eusebio
da Silva Ferreira alikuwa mfungaji bora wa fainali za Kombe la Dunia
zilizofanyika nchini England mwaka 1966 kuanzia Julai 11, hadi Julai 30
wenyeji England wakiifunga Ujerumani Magharibi 4–2 na kutwaa Kombe.
Eusebio
alifunga mabao tisa na kuwapiku Helmut Haller mabao sita, Geoff Hurst,
Franz Beckenbauer, Ferenc Bene na Valeriy Porkujan mabao manne kila
mmoja na Luis Artime na Bobby Charlton waliofunga matatu kila mmoja.
Eusebio
aliyezaliwa Januari 25, mwaka 1942, anachukuliwa kama mchezaji bora
daima kuwahi kutokea duniani na Shiriksiho la Viwango la Kimataifa
(IFFHS). Aliisaidia Ureno kushika nafasi ya tatu kwenye fainali hizo kwa
mabao yake hayo, sita akifunga kwenye Uwanja wa Goodison Park na
kuchaguliwa kuwa Mwanasoka Bora Ulaya mwaka 1965. Aliichezea Benfica kwa
miaka 15 na ndiye mfungaji bora daima wa klabu hiyo.
Pumzika kwa amani Eusebio |
No comments:
Post a Comment