Mshambuliaji
wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski atajiunga na klabu ya Bayern
Munich kwa uhamisho huru mwishoni wa mwa msimu huu, mabingwa wa
Ujerumani wametangaza.
Mshambuliaji huyo wa Poland, ambaye aliisadia Dortmund kushinda makombe mawili mfululizo ya Bundesliga 2011 na 2012, amesaini mkataba wa miaka mitano.
Mshambuliaji huyo wa Poland, ambaye aliisadia Dortmund kushinda makombe mawili mfululizo ya Bundesliga 2011 na 2012, amesaini mkataba wa miaka mitano.
Lewandowski
alitangaza nia yake ya kuondoka Westfalenstadion pindi mkataba wake
utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu, na akawa anahusishwa na kujiunga
na wapinzani wao Bayern.
Lewandoski,
25, alijaribu kulazimisha kuuzwa kipindi cha kiangazi kilichopita
lakini Dortmund waligoma kumuuza na kusisitiza lazima amalize mkataba
wake.
Mwenyekiti
wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alitangaza dili la Lewandoski, akisema:
"Tuna furaha uhamisho huu umekamilika kwa mafanikio.
"Robert Lewandowski ni mmoja ya washambuliaji bora ulimwenguni, atakiongezea ubora kikosi chetu cha FC Bayern."
No comments:
Post a Comment