Sunday, January 12, 2014

HATIMAYE MAN UNITED YAZINDUKA YAICHAPA SWANSEA 2-0

KOCHA David Moyes amepumua kidogo baada ya Manchester United kushinda 2-0 dhidi ya Swansea City usiku huu Uwanja wa Old Trafford na kuepuka kipigo cha nne mfululizo na cha tatu Uwanja wa nyumbani. 
Ushindi wa United leo katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England umetokana na mabao ya Antonio Valencia dakika ya 47 na Dany Welebeck dakika ya 59
United sasa inatimiza pointi 37 baada ya kucheza mechi 21, ingawa inabaki nafasi ya saba kwenye msimamo.

Ahead: Valencia celebrates after putting United 1-0 up just after the break at Old Trafford

No comments:

Post a Comment