Sunday, January 12, 2014

YAYA TOURE NDIYO BABA LAO AFRIKA

Mchezaji wa Manchester City ambaye pia hucheza nafasi ya kiungo cha kati katika timu ya Ivory Coast, Yaya Toure ndiye mwanasoka bora zaidi mwaka 2013 barani Afrika
Toure alikabidhiwa tuzo la (caf) mwaka wa tatu mfululizo katika sherehe zilizofanyika mjini Lagos, Nigeria Alhamisi usik

Aidha Toure pia alishinda tuzo la BBC la mwanasoka bora zaidi barani Afrika mwaka jana.
Alikuwa anawania tuzo hilo dhidi ya mchezaji mwenzake wa Ivory Coast Didier Drogba, ambaye huchezea Galatasaray na John Mikel Obi mnigeria ambaye husakata soka nchini Uingereza.

"nimefurahi sana kwa sababu hii ni ishara kuwa nacheza vyema sana ,'' alisema Toure baada ya kupokea tuzo yake.
Lakini alisema kuwa majaji walikuwa na wakati mgumu kumchagua mchezaji bora kwa sababu washindani wenzake wote ni wazuri.

''Sikudhani kama nitashinda kwa sababu Drogba na Obi Mikel ni wasakataji wazuri wa kabumbu,'' aliongeza Toure.
Washidi wa hivi karibuni wa tuzo ya Caf
2013 Yaya Toure
2012 Yaya Toure
2011 Yaya Toure
2010 Samuel Eto'o
2009 Didier Drogba
2008 Emmanuel Adebayor
2007 Frederic Kanoute
2006 Didier Drogba 


Abedi Pele wa Ghana alishinda tuzo hiyo mara tatu kati ya mwaka 1991-93 huku Samuel Eto'o akishinda kati ya mwaka 2003-05.

Bila shaka klabu ya Man City anakosakatia kambumbu Toure, bado haishinda kombe lolote la klabu lakini nyota yake imekuwa iking'aa sana nyumbani na katika nyanja za kimataifa.

Toure ndiye mchezaji pekee wa kiafrika kuwa katika orodha ya wachezaji 23 walioteuliwa kuwania tuzo la mchezaji bora la FIFA mwaka jana.

Mshindani wake wa karibu aliyekuwa pia anawania tuzo la Caf, Mikel, mwenye umri wa miaka 26, alisaidia Nigeria kushinda kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment