KLABU ya Manchester United inataka kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon ya Ureno, William Carvalho.
United
imekuwa ikisaka kiungo mkabaji sehemu mbalimbali na kwa mara nyingine,
wasaka vipaji wake walishuhudia mechi ambayo Sporting ilitoka sare ya
0-0 na Porto jioni ya Jumapili, kwa mujibu wa A Bola.
Taarifa
nchini Ureno zinasema kwamba, United sasa tayari imekwishamshuhudia
mchezaji huyo katika mechi saba za mzunguko wa kwanza, na kocha David
Moyes anamtaka kuimrisha safu yake ya kiungo.
Katikati ya dimba: Carvalho ana thamani ya Pauni Milioni 37.5, ingawa United wanamtaka kwa bei poa
No comments:
Post a Comment