MRENO Cristiano Ronaldo amemtambia kwa
mara nyingine, Msweden Zlatan Ibrahimovic, baada ya Real Madrid kuifunga
bao 1-0 PSG katika mchezo wa kirafiki wa majira ya baridi mjini Doha.
Jese alifunga bao hilo pekee dakika ya19
na kumfanya Ronaldo aliyemnyanyasa Ibra katika mechi za kufuzu Kombe la
Dunia mwishoni mwa mwaka jana akiiwezesha Ureno kushinda mechi zote
dhidi ya Sweden nyumbani na ugenini, aendeleze ubabe wake kwa mwenzake.
Mshambuliaji huyo kinda mwenye umri wa
miaka 20, ambaye amebukia kwenye timu ya vijana ya vigogo hao wa
Hispania, hadi sasa amecheza mechi 16 na kuifungia mabao mawili timu
hiyo.
Kifaa: Jese (wa pili kushoto na chini) akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi
Ibrahimovic alitaniana na kocha Carlo Ancelotti wakati wa mapumziko
Ibrahimovic na Ronaldo (chini) walikuwa nyota wa mchezo leo
Ibra akiruka kumzidi Ronaldo kupiga mpira kichwa katika mchezo wa kirafiki Doha
Ronaldo akiwatoka mabeki wa PSG
No comments:
Post a Comment