Ujumbe
wa kutoka nchini Cameroon wanatarajiwa kwenye nchi za Ulaya kuwashawishi
wachezajiwa wa nchi hiyo wanachezea katika nchi za ulaya kujiunga na
timu ya taifa ya nchi hiyo "Indomitable Lions".
Mpango huo wa kusaka vipaji vipya umekuja wakati
Cameroon ikiwa inajiandaa kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka
kesho nchini Brazil
Chama cha soka cha Cameroon -
Fecafoot kimesema mpango wao kwa sasa ni kushawishi wachezaji wanne
wanaocheza soka ya kulipwa nchini Ufaransa.
Wachezaji hao Axel Ngando anachezea klabu ya
Auxerre ya ligi daraja la pili nchini Ufaransa, Samuel Umtiti anachezea
Lyon na Jean- Christophe Behebeck anachezea Valenciennes.
Mchezaji mwinginie anayewindwa ili kuuongeza
nguvu kwenye timu ya taifa ya Cameroon ni Paul Geoges Ntep de Madiba
ambaye pia naye anayechezea Auxerre ya Ufaransa.
Tunataka kuwashawishi hao wachezaji wachezee
timu ya taifa ya Cameroon, na hasa kwenye fainali za Kombe la Dunia na
pia wachezee Cameroon kwa hapo baadae Shirikisho la soka la Cameroon
limesema kwenye taarifa yake.
No comments:
Post a Comment