Sunday, January 26, 2014

ZAHA , FABIO KWENDA CARDIFF CITY KWA MKOPO

WACHEZAJI wawili wa Manchester United, Wilfried Zaha na Fabio Da Silva wapo karibu kujiunga na Cardiff City.
Winga wa United, Zaha amekwenda kufanyiwa vipimo vya afya St George Park kuekelea kukamilisha uhamisho wa mkopo hadi mwishoni mwa msimu, wakati bek Fabio anatarajiwa kusaini Mkataba wa moja kwa moja.
Zaha amekuwa akitakiwa na Cardiff tangu Oktoba na sasa ndoto za klabu hiyo kumpata nyota huyo zinatimia.    



No comments:

Post a Comment