KOCHA
Jose Mourinho amewabwatukia Barcelona kuwatia presha kuelekea mechi yao
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya leo dhidi ya Manchester City.
Mwalimu
huyo wa Chelsea, ambaye alishuhudia timu yake ikifungwa Uwanja wa
Etihad katika Kombe la FA mwishoni mwa wiki, amesema Barca ya sasa ni
mbovu mbovu ukilingalinganisha na miaka kadhaa iliyopita.
Cha mdomo; Jose Mourinho amesema Man City inakutana na Barca 'mbofu mbofu' |
Hasira za Leo: Nyota wa Barcelona, Lionel Messi akiwa mazoezini Uwanja wa Etihad jana
Wakati
kikosi cha Gerardo Martino hakiachani mbali sana na Real na Atletico
Madrid katika mbio za ubingwa wa La Liga, lakini wanaonekana bado wapo
imara katika michuano ya Ulaya.
Wametua
Manchester jana asubuhi kwa ajili ya mchezo huo wa hatua ya 16 Bora
Ligi ya Mabingwa. Licha ya kutemeshwa taji na mabingwa wa Ulaya wa sasa
Bayern Munch msimu uliopita, bado wana nia ya kushinda tena mjini
Lisbon.
Messi na wachezaji wenzake wa Barcelona mazoezini Etihad
No comments:
Post a Comment