KINDA Adnan Januzaj amepigiwa simu na Naibu Waziri Mkuu wa Kosovo kuombwa aichezee mechi ya kwanza ya kimataifa nchi hiyo.
Behgjet
Pacolli, bilionea mmiliki kampuni za ujenzi anayekadiriwa kuwa na
utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 550, anajaribu kumshawishi Januzaj
acheze dhidi ya Haiti mwezi ujao.
Januzaj,
mwenye umri wa miaka 19, badohajaamua acheze nchi gani soka ya
kimataifa, lakini familia yake ilikuwa moja ya wanaharakati wa uhuru wa
nchi hiyo.
Wito Kosovo: Kosovo imemkaribisha mchezaji wa Manchester United, Adnan Januzaj aichezee timu yao ya taifa
Pamoja
na hayo, Kosovo bado haijapata uanachama wa FIFA, wameruhusiwa kucheza
mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Haiti mwezi ujao.
Januzaj alizaliwa mjini Brussels, Ubelgiji lakini kuna utata mkubwa juu ya mustakabali wake katika soka ya kimataifa.
England ni moja ya nchi ambazo zinatumaini kumpata Januzaj.
Tishio
jipya: Januzaj alianza kutisha katika Ligi Kuu ya England mapema msimu
huu kwa kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-1 wa United dhidi
ya Sunderland
No comments:
Post a Comment