Saturday, May 23, 2015

RATIBA MICHEZO YA MWISHO LIGI KUU ENGLAND - SEASON 2014-2015

Sunday 24 May 2015

IN CAT
 
Stoke CityvLiverpoolBritannia Stadium16:00
Newcastle UnitedvWest Ham UnitedSt. James' Park16:00
Manchester CityvSouthamptonEtihad Stadium16:00
Leicester CityvQueens Park RangersKing Power Stadium16:00
Hull CityvManchester UnitedThe KC Stadium16:00
EvertonvTottenham HotspurGoodison Park16:00
Crystal PalacevSwansea CitySelhurst Park16:00
ChelseavSunderlandStamford Bridge16:00
Aston VillavBurnleyVilla Park16:00
ArsenalvWest Bromwich AlbionEmirates Stadium16:00

NDEMLA, ISIHAKA HASSANI WAONGEZA MKATABA SIMBA






BEKI aliyewahi kuripotiwa kutakiwa na Real Madrid Castilla, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Hispania, maarufu kama Segunda B, Hassan Isihaka (pichani kulia) amesaini Mkataba mpya wa miaka mitatu na Simba SC.
Mapema mwaka huu, maskauti wa Real Madrid waliozuru Tanzania, walivutiwa na wachezaji wawili wa SImba SC, beki Isihaka Hassan na kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’.

Timu hiyo ya pili ya mabingwa wa Ulaya, Real Madrid inayocheza mechi zake Uwanja wa Alfredo di Stefano, kupitia mwakilishi wake, Rayco Garcia iliwasilisha rasmi maombi yake kwa klabu ya Simba SC juu ya wachezaji hao.

Garcia alisema anawataka wawili hao Juni mwaka huu waende Hispania kufanyiwa majaribio katika timu hiyo na kama wakifuzu wataanza maisha mapya Ulaya.

Wakati bado Juni inabisha hodi, Isihaka anarefusha muda wa kuendelea kuitumikia Simba SC hadi mwaka 2018.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema  jana kwamba, mbali na Isihaka, kiungo chipukizi Said Hamisi Ndemla naye ameongeza Mkataba wa miaka mitatu pia.
“Chipukizi hawa wawili, wote wataendelea kufanya kazi Simba SC hadi mwaka 2018, na bado tunapitia ripoti ya benchi la Ufundi, ili kuboresha mikataba ya wachezaji wengine ambao tunahitaji kuendelea nao,”amesema Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

FLANAGAN , IBE WASAINI KANDARASI MPYA NDANI YA LIVERPOOL

Wachezaji kinda wa Timu ya liverpool Jordan Ibe na Jonh Flanagan hatimae wamesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo  hadi mwaka 2020.

TAIFA STARS HOVYOOOOOOOO

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jana ilipandishwa virago na kurejea Tanzania baada ya kupokea vichapo vitatu mfululizo kutoka kwa swazland,madagascar na lesotho.

Timu hiyo dhaifu kuwahi kutokea katika michuano hiyo aambayo walienda kushiriki kama waalikwa wakiwemo na timu ya taifa ya Ghana. Stars alioongozwa na Cap[tain wao John Bocco  baada ya kuchukua kitambaa hiko kutoka kwa Nadir Haroub amabaye ni majeruhi.

Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanasema kwamba timu hiyo si ya taifa ni TFF kwani uteuzi wake ulifanywa kwa magumashi na kutoangalia uwezo wa mchezaji katika ligi iliyoisha hivi karibuni.

Kuna wachezaji wengi ambao wameonyesha kiwango kikubwa kama Salum Telela, Jonas Mkude, Hassani Kessy, Malimi Busungu, Rashidi Mandawa, David luhende  na wengineo wengi ambao wameonyesha kiwango kizuri, cha kushangaza wachezaji hao hawakuitwa na matokeo yake wameitwa wachezaji majeruhi na walioshuka kiwango hivi karibuni mfano, Kazimoto, John Bocco, Saidi juma, oscar Josha, Erasto Nyoni,.

Kwa mujibu wa mashabiki walioambatana na timu hiyo huko Afrika Kusini, wanasema kwamba sababu ya timu hiyo kufanya vibaya ni kutokuwa na ushirikiano baadhi ya viongozi walioambatana na timu hiyo na kwamwe timu haiwezi kufanya vizuri.