Kufuatia kuondoshwa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika
hatua ya 16 bora, klabu ya Yanga imeangukia kwenye michuano ya kombe la
Shirikisho Afrika. Kwa mujibu wa kanuni za CAF, vilabu vyote
vinavyotupwa nje ya mashindano ya klabu bingwa Afrika vinakutana na
washindi wa hatua ya 16 bora ya kombe la shirikisho kukipiga mchezo wa
playoff unaoamua timu gani inasonga mbele kwenye hatua ya makundi katika
kombe la shirikisho.
Usiku wa Jumatano Yanga ilisukumwa nje ya kombe la mabingwa Afrika na
klabu ya Al Ahly ya Misri kwa kufungwa magoli 2-1 ugenini hivyo
kuenguliwa kwenye michuano hiyo kwa jumla ya magoli 3-2 baada timu hizo
kutoka sare ya kufungana goli 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa
Dar.
April 21 imechezeshwa droo ya kuamua ni timu gani zitakutana
kwenye mechi za mchujo zitakazoamua ni timu gani zitafuzu hatua ya
makundi ya kombe la shirikisho Afrika.
Mabingwa watetezi wa VPL Yanga wamepangwa kucheza na klabu ya Sagrada
Esparanca ya Angola ambapo Yanga wataanzia nyumbani mchezo wa kwanza
(uwanja wa taifa, Tanzania) kati ya May 6-8 huku mchezo wa marudiano
ukipangwa kufanyika Angola kati ya May 17-18, 2016.
No comments:
Post a Comment